UFAHAMU UGONJWA WA KIFAFA NA TIBA YAKE
Na _Dr Peter_ Huu ni ugonjwa ambao unasabababishwa na seli zilizopo katika mishipa ya fahamu zilizopo kwenye ubongo kutoa umeme [impulses] mwingi kuliko kawaida kwenda kwenye misuli na sehemu zingine za mwili, na kusababisha mtu kupata dalili kama vile kuishiwa nguvu, kichwa kuuma, kuchanganyikiwa, mwili kukakamaa na hata kupoteza fahamu. Hali hii hujirudia mara kwa mara. Ifahamike kuwa, aina ya kifafa inayojulikana sana mitaani ni ile ambayo mtu anakakamaa na kupoteza fahamu, japokuwa kuna aina za kifafa ambazo mtu hakakamai wala kupoteza fahamu, kama tutakavyoona hapo baadae. Mwaka 2013 ugonjwa huu uliua zaidi ya watu laki moja duniani, 80% wakiwa waafrika. Mgonjwa huyu huweza kuanguka mara kadhaa kwa mwezi lakini anaweza asianguke kabisa kama anafuata masharti na utaratibu mzuri wa matibabu… Chanzo cha ugonjwa wa kifafa ni nini? chanzo kikuu cha ugonjwa huu kwa watu wengi hua hakifahamiki lakini baadhi ya hiz ni moja ya sababu za kuugua kifafa. Kurithi; familia na k...