NJIA KUU MBILI ZA KUPATA MAPACHA
Dr _Peter_
Zipo njia zinazokuwezesha kupata mapacha, kwanza ni jinsi ya kupata mapacha bila dawa au tiba yoyote na pili ni jinsi ya kupata mapacha kwa kutumia dawa au tiba maalum. SASA ENDELEA…
Tukianza kuangalia njia ya kwanza, katika njia hii zipo sababu mbalimbali, kwanza ni umri; umri mkubwa wa zaidi ya miaka 30 huchangia mwanamke kupata mapacha, hii ni kwa sababu kiwango cha homoni ya FSH au Follicle Stimulating Hormone husaidia katika kuendeleza mayai katika ovari au vifuko vya mayai kabla hayajatoka. Katika kipindi hiki mayai hutoka zaidi ya moja na husababisha kutokea kwa mimba za mapacha.
Historia ya kuwepo mapacha katika familia pia huchangia. Kwa kawaida kuna aina mbili za mapacha, kwanza ni mapacha watokanao na yai moja na pili ni mapacha wa mayai mawili tofauti. Kupata mapacha wa yai moja au identical twins haimaanishi katika uzao wako utaendelea kupata mapacha. Endapo utapata mapacha wa mayai mawili tofauti- fraternal twins, basi uwezekano wa kupata mapacha unakuwa mkubwa kama upande wa baba au wa mama kuna aina hizi za mapacha.
Mapacha wa yai moja ni aina ya mapacha ambao hufanana sana na huwezi kuwatofautisha na wote huwa wa jinsia moja. Mapacha wa mayai mawili tofauti huwa hawafanani sana na wanaweza kuwa wa jinsi moja au jinsi tofauti yaani wa kike na wa kiume. Historia ya kuwa na mapacha katika familia ya upande wa mwanamke hasa katika hili la fraternal twins huchangia kuongeza nafasi ya uweo wa mapacha katika familia.
Vilevile uwepo wa mapacha wa fraternal au wa mayai mawili tofauti kwa mwanaume huchangia uwepo wa uwezo wa mwanaume kutoa mbegu nyingi sana zenye ubora na zenye uwezo wa kurutubisha yai zaidi ya moja. Uzito mkubwa au unene mkubwa kwa wanawake (obesity) ambao hufikia BMI zaidi ya 30 husababisha wanawake wapate ujauzito wa mapacha kulinganisha na wanawake walio na afya nzuri yaani siyo wanene.
Changamoto iliyopo hapa ni kwamba wanawake wanene pia hupata matatizo makubwa ya uzazi kwani wengi hushindwa kupata mimba kutokana na tatizo liitwalo PCOD. Mwanamke mnene ni rahisi kupata mapacha kutokana na uwepo wa mafuta ya ziada mwilini mwaka ambao huzalisha kichocheo cha estrogen, kiwango cha juu cha estrogen mwilini huchochea utokaji wa mayai mengi.
Over stimulation ambapo hutoka mayai zaidi ya moja. Wanawake warefu zaidi kuliko wengine kwenye ile jamii wapo katika uwezekano wa kupata mimba ya mapacha. Mwanamke huwa na uzao mkubwa yaani kuzaa watoto zaidi ya watano, basi upo uwezekano baada ya hapo kupata mapacha. Utaifa nao huchangia kwa kiasi kupata
mapacha, wanawake wa kitaifa wanaongoza kupata mapacha ni Waamerika na mwisho ni wa mataifa ya Asia.
Tafiti pia zinaonesha kwamba wanawake wanaopata mimba wakiwa bado wananyonyesha wana nafasi kubwa ya kupata mimba ya mapacha kulinganisha na wale ambao hawanyonyeshi.
Unywaji wa maziwa ya ngombe na products nyingine za maziwa haya mara kwa mara au kwa kupata mimba ya mapacha kutokana na kwamba kwenye maziwa ya ng’ombe kuna kichocheo kipo kwa kiasi kikubwa husaidia kuamsha mayai mengi kwa mwanamke.
Njia za TiBa
Njia nyingine za kupata mapacha ni kutumia dawa za virutubisho ambazo zinarutubisha mayai na kufanya mayai ya mwanamke yaweze kupevuka mawili mawili na hatimae kupata Pacha.
Wasiliana nasi
Eden Herbal and Health Care
0755638056
0784467374
Comments
Post a Comment