TATIZO LA JOGOO KUSHINDWA KUWIKA- Erectile Dysfunction
Na _Dr Peter_
Kuna tatizo ambalo wengi huwa tunaliita ukosefu wa nguvu za kiume. Neno hili kama linavyotumika mimi naliona ni pana mno na halielezei hasa ni kitu gani kinamaanishwa kwani kuna matatizo lukuki ambayo yote yapo katika kundi la ukosefu wa nguvu za kiume. Leo tutazame tatizo ambalo limeliita tatizo la jogoo kushindwa kuwika au jongoo kushindwa kupanda mtungi. Kwanza tutazame muundo wa uume na nini kinatokea pale uume unaposimama.
Uume ni kiungo cha uzazi cha mwanamme. Uume ina sehemu moja ndefu kuliko nyingine na mwishoni kuna kichwa (glans). Tundu lililopo kwenye kichwa (meatus) ni kwa ajili ya kutolea mkojo.
Ndani ya uume kuna vyumba viwili vyenye umbo la silinda vinacyoitwa corpora cavernosa vinavyotambaa urefu wote wa dhakari. Vyumba hivi vina uwingi wa mishipa ya damu. tishu na vifuko vya wazi. Mrija wa kupitisha mkojo na shahawa (urethra) unatambaa chini ya corpora cavernosa, ndani ya tishu zilizo kama sponji ziitwazo corpus spongiosum.
Ateri kuu mbili (moja ndani ya kila corpora cavernosa) na veni kadhaa zinatiririsha damu ndani na nje ya uume. Neva hupeleka taarifa kutoka na kwenda sehemu nyingine za mwili.
Nini Maana Ya Jogoo Kuwika (Uume kusimama)?
Tendo la uume kusimamam huanzia ndani ya ubongo. Kutokana na kitu ulichokiona, ulichogusa, kunusa, kusikia au kuwaza, neva hupeleka taarifa za kikemikali kwenye mishipa ya damu iliyo ndani ya uume. Ateri zitalegea na kufunguka ili kuruhusu damu nyingi zaidi iingie, wakati huo huo veni zitaziba. Damu ikishakuwa ndani ya uume, msukumo huifanya damu inase ndani ya corpora cavernosa. Uume utatanuka na kuufanya uume usimame kwa muda mrefu.
Damu ikiacha kuingia ndani ya uume, veni zinafunguka, na uume unalegea.
Nini Maana Ya Jogoo kushindwa kupanda mtungi?
Hii ni hali inayomtokea mwanamme ambapo anakuwa na hamu ya kufanya tendo la ndoa lakini uume wake hausimami kabisa, kukosa kusimama kikamilifu au kusimama kikamilifu kwa muda mfupi sana hivyo kukosa nguvu ya kufanya tendo lililokusudiwa. Nusu wa wanaume hupata tatizo hili wanapofikia umri wa miaka 40, idadi ikiongezeka kwa wanaume wenye umri mkubwa zaidi, kwa mfano asilimia 70 ya wanaume wenye miaka 70 huwa na tatizo hili. Ifahamike kwamba kila mmoja wetu huweza kupata tatizo hili kwa muda fulani kutokana na vitu kama uchovu, kupata kilevi, punyeto, kutoelewana na mwenzi n.k. Tunasema mwanamme ana tatizo hili pale hali hii inapoendelea kwa kipindi kirefu, kwa mfano hali hii ikitokea kwa mwezi mzima mfululizo.
Sababu
Mambo mengi husababisha tatiz hlo, tendo la uume kusimama linahusisha ubongo, homoni, misuli na mishipa ya damu, tatizo katika hayo ndilo linaloweza kusababisha jongoo ashindwe kupanda mtungi.
Baadhi ya sababu zinapelekea uume kutosimama au uume kukosa nguvu ni:
Magonjwa ya moyo na kusinyaa kwa mishipa ya damu
Unene wa kupindukia
Ugonjwa wa kisukari
Uvutaji wa sigara
Utumiaji wa pombe
High blood pressure
Cholesterol nyingi katika damu
Ugonjwa wa Parkinson’s
Ugonjwa wa multiple sclerosis
Upungufu wa homoni ya testosterone
Tiba ya tezi dume
Kuumia kwenye nyonga au uti wa mgongo
Tiba ya mionzi kwenye eneo la nyonga
MADHARA
Kuna madhara mengi yanayotokana na tatizo la jongoo kushindwa kupanda mtungi. Mwanamme anayepatwa na tatizo hili hushindwa kumridhisha mwenzi wake na hali hii huwezauume kushindwa kusimamakusababisha matatizo makubwa katika mahusiano ya kimapenzi au katika ndoa. Hali hii hupelekea mwanamme huyu kuanza kuwa na wasiwasi na msongo wa mawazo, huanza kukosa kujiamini na kujiona ana mapungufu. Tatizo hili pia linasababisha mwanamme huyu ashindwe kumpa ujauzito mkewe.
Ifahamike kwamba uume kusimama maana yake damu kuingia katika kiungo hicho, hivyo tiba ya uume kutosimama ni kutafuta njia ya kufanya damu ifike kwenye kiungo hicho kwa kiasi kinachotakiwa. Hii ni pamoja na kuondoa matatizo ya moyo, kupunguza unene, kupunguza cholesterol na kutumia dawa za kufungua njia za mishipa ya damu.
Ipo mimea mingi iliyothibitishwa kuwa inasaidia au kuponya kabisa tatizo la jongoo kushindwa kupanda mtungi na tumekuwa tukiitumia kwa mafanikio makubwa mimea hiyo imekuwa ikitengeneza dawa. Dawa hizo hupatikana kama vidonge au unga ambao hutumiwa kwa kunywewa kama chai au kahawa. Mimea maarufu iliyothibishwa ni pamoja na epimedium, ginseng na rhodiola rosea.
Dawa Bora ambayo inatumika Sana Kwa sasa na ambayo inaleta mafanikio makubwa katika kuondoa matatizo yanayowasumbua wanaume ni *LuvPunch*. Dawa hii inatokana na mimea ya Semen Cuscutae, Fructus Lycii, Rhixoma Diocoreae, Radix Rehmanniae Preparata na Cortex Moutan. Dawa hii huanza kuleta mabadiliko mwilini kwa muda mfupi sana na kumwezesha mwanamme kumudu tendo la ndoa, mara nyingi zaidi.
LuvPunch humwongezea uwezo wa kufanya tendo la ndoa mwanamme kwa:
1. Kuboresha figo
2. Kuongeza uwingi wa manii (Sperm count), kuongeza uwezo na kasi ya kutembea ya manii (Sperm Motility)
3. Kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanamme
4. Kuongeza uwingi wa oksijeni katika damu na kusaidia uume kusimama imara
5. Kuondoa tatizo la kuwahi kufika kileleni (Premature Ejaculation)
6. Kuondoa tatizo la jogoo kushindwa kuwika (Erectile Dysfunction)
7. Kuondoa tatizo la manii kutoka yenyewe pasipotarajiwa.
Jee, una tatizo la jongoo kushindwa kupanda mtungi na ungependa kupata maelezo ya kina zaidi au kusaidiwa kupata dawa za kutumia? Usisite kuwasiliana nasi.
Kwa mawasiliano zaidi tuma ujumbe wako kupitia whatsapp namba 0755638056/au yupigie 0784467374
Eden Herbal & HealthCare
Comments
Post a Comment