FAHAMU KUHUSU TATIZO LA CHUNUSI (ACNE)
🌴 Eden Herbal and Health Care🌴
Chunusi ni ugonjwa wa ngozi unaowaathiri watu wengi. Ugonjwa huu husababisha vipele vidogo vidogo vya mafuta kwenye ngozi na wakati mwingine hufanya ngozi kuwa na maumivu au kuhisi kuungua. Viupele hivi hutokea wakati vishimo vya kupitisha jasho katika ngozi vinapozibwa kwa mafuta na seli za ngozi zilizokufa au bakteria. Mara nyingi chunusi hutokea usoni, mgongoni, kifuani na shingoni. Chunusi huwaathiri takribani asilimia 80% ya watu wenye umri kati ya miaka 11-30. Ugonjwa huu hutokea zaidi wasichana kuanzia miaka 14-17 na wavulana kuanzia miaka 16-19.
Chunusi hutokea jinsi gani?
Kawaida ngozi ina vishimo vidogo vidogo vya kutolea jasho,mafuta na seli zilizozeeka kutoka ndani ya mwili. Katika ngozi pia kuna tezi ya mafuta iitwayo ‘sebacous gland’ inayotoa mafuta yaitwayo sebum. Uzalishaji wa sebum nyingi na seli za ngozi zilizokufa husababisha kuziba kwa vishimo vidogo vidogo vya ngozi vinavyopitisha jasho katika ngozi na kusababisha kuvimba na mara nyingine kujaa kwa usaa na kusababisha chunusi. Chunusi pia husababishwa na mabadiliko ya homoni, matibabu au kurithi(genetics).
Kwa matibabu na ushauri wasiliana nasi Eden Herbal Clinic
0745 859 915
0759 359 747
0755 638 056
Comments
Post a Comment