🌳 VIDONDA VYA TUMBO NA TIBA YAKE🌳



Na _Dr Peter_

⚡Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ni mfumo unaohusika na umeng'enyaji wa chakula mpaka kuwa katika hali inayoweza kusharabiwa na mwili.
⚡Sehemu kuu zinazohusika katika umeng'enyaji huo ni kinywa, umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach', ini, mfuko wa nyongo, utumbo mwembamba 'Duedenum & Ileum', kongosho, utumbo mpana na puru 'Rectum'.
⚡Mfumo wa mmeng'enyo wa chakula hasa kuta za umio, tumbo na utumbo mwembamba hupata mmomonyoko ambao husababishwa na asidi inayotumika kumeng'enya chakula inaposhambulia kuta hizo. Kitaalamu hali hii hutambulika kama 'Peptic ulcers'.
Stomach Ulcers
Vidonda vya mfumo wa umeng'anyaji chakula, vikiwa kwenye tumbo tunaita vidonda vya tumbo 'Gastric ulcer', vikiwa katika duodenum tunaita 'Duodenal ulcer' na vikiwa katika esophagus tunaita 'Esophageal ulcer'

SABABU ZA KUWA NA VIDONDA VYA TUMBO☘
👉Bakteria aina ya Helicobacter pylori 'H.pylori' & Non-Steroidal Anti Inflammatory Drugs 'NSAIDs' ndio visababishi vikuu.
👉Bakteria H.pylori wanahusika sana kwa angalau nne ya tano ya vidonda vya tumbo 'Gastric ulcers' & 95% ya 'Duodenal ulcers' ambapo NSAIDs husababisha 20% ya 'Gastric ulcers' na 5% ya 'Duodenal ulcers'
👉Bakteria H.pylori husababisha kupitia vyakula na maji. Pia hupatikana kwenye mate ya binadamu hivyo inaweza kusambazwa mdomo kwa mdomo wakati mkila denda/kunyonyana midomo.
👉Bakteria H.pylori huishi kwenye kuta za utumbo na hutengeneza vimeng'enya 'Enzyme' iitwayo 'Urease' inayopunguza athari za asidi kwenye utumbo.
👉Utumbo hutaka kufidia kiasi cha asidi kinachopotea kwa kutengeneza zaidi na husababisha kukwangua kuta za utumbo.
👉Non-Steroidal Anti Inflammantory Drugs 'NSAIDs' ni dawa za kutuliza maumivu ya kichwa, maumivu ya hedhi, kushusha homa na kuondoa maumivu madogo madogo mfano Aspirin, Ibuprofen,Diclofenac & Meloxicam. Dawa hizi hupunguza uwezo wa kuta za tumbo na kufanya uwe rahisi kushambuliwa na asidi za tumboni hivyo kusababisha vidonda.
👉Chembe za urithi 'Genetics': Idadi kubwa ya watu wenye vidonda vya tumbo wana ndugu wa karibu wenye vidonda pia, hii huwafanya wataalamu kufikiria kuwa chembe za urithi zinahusika pia.
👉Uvutaji sigara/tumbaku: Wavutaji wa sigara wako katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiovuta.
👉Matumizi ya pombe/vilevi: Walevi wako katika hatari zaidi ya kupata vidonda vya tumbo ikilinganishwa na wasiotumia vileo/pombe.
👉Msongo wa mawazo 'Mental stress': Msongo wa mawazo hausababishi vidonda moja kwa moja ila hufanya hali kuwa mbaya zaidi kwa wagonjwa.

🌿DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO🌿
⚡ Maumivu ya tumbo na huwa makali zaidi pale asidi inapopita juu ya vidonda.
...Maumivu yanaweza anzia kwenye kitovu na kupanda juu hadi katikati ya kifua 'Epigastric pain'
...Maumivu yanaweza kuongezeka unapokuwa njaa. Pia yanaweza kuwa makali wakati wa usiku kwenye mida ya kulala, yanayoweza kupunguzwa kwa kula chakula kidogo.
⚡ Kushindwa kumeza vizuri chakula.
⚡ Chakula kukwama kama kinataka kurudi mdomoni.
⚡ Kujisikia vibaya baada ya kula.
⚡ Kupungua uzito.
⚡ Kukosa hamu ya kula.

🌴DALILI HATARI🌴
⚡Kutapika damu.
⚡ Kupata choo kikubwa cheusi au chenye damu nzito.
⚡ Kichefuchefu & kutapika.

JINSI VIDONDA HUGUNDULIWA:-
Maelezo ya mgonjwa juu ya dalili alizonazo humsaidia daktari kuhisi kinachomsumbua mteja wake ni vidonda vya tumbo.

Ili kuthibitisha vidonda vipimo vifuatavyo hufanyika :-

_Kupima damu 'Blood test'_
Kuangalia bakteria aina ya H.pylori na kama mgonjwa amekuwa akitumia antibayotiki au dawa za vidonda Proton Pump Inhibitors 'PPIs' mfano Omeprazole vipimo vyake vya damu vitaonyesha majibu hasi 'Negative'

_Kupima pumzi 'Breath test'_
Mgonjwa hupewa anywe maji yenye atomi za kaboni zinazoweza kuvunjika, hii hufanya bakteria H.pylori kuvunjika na baada ya lisaa mgonjwa hutoa pumzi kwenye chombo kilichofunikwa kama mgonjwa ameambukizwa sampuli ya pumzi itaonyesha vipande vya kaboni kwenye kabonidioksaidi.

_Kupima antijeni kwenye kinyesi 'Stool antigen test'_
Kipimo hiki huangalia kama kuna bakteria H.pylori kwenye kinyesi.  Vilevile kipimo hiki hutumika kuangalia ufanisi wa matibabu yaliyotolewa dhidi ya bakteria.

_X-ray ya sehemu ya juu ya tumbo 'Upper gastrointestinal x-ray'_
Picha huonyesha umio 'Esophagus', mfuko wa tumbo 'Stomach' na Dudenum. Mgonjwa humeza maji yenye 'Barium' ambayo hufanya vidonda kuonekana kirahisi kwa x-ray.

_Kamera ya tumbo 'Endoscopy'._
Mrija mrefu wenye kamera huingia tumboni na daktari huona vidonda kwenye skrini ya kompyuta 'Monitor'.

⚡MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO⚡
Kama vidonda vitakuwa vimesababishwa na bakteria H.pylori dawa za kuua na kuondoa bakteria hutumiwa.

Kama vidonda vya tumbo vitakuwa vimesababishwa na 'NSAIDs' na hana maambukizi ya bakteria H.pylori atapaswa kutumia dawa Proton Pump Inhibitors 'PPIs'

Proton Pump Inhibitors 'PPIs' hufanya kazi kwa kuvunja/kuzuia kazi ya protini ziitwazo 'Proton Pump' ambazo huhusika katika utengenezaji wa asidi tumboni.

Matumizi ya NSAIDs kwa ajili ya kuondoa homa na maumivu yatarithiwa na dawa kama Paracetamol.

Matibabu yaliyozungumziwa hapo juu yanaweza kuchukua muda kabla ya kuanza kufanya kazi hivyo daktari anaweza kuongeza matibabu mengine kama vizuia asidi 'Antiacids' & 'Alginates' kwa ajili ya nafuu ya haraka.

Usitumie dawa hizi ndani ya lisaa moja baada ya kunywa PPIs mfano Omeprazole au H2-Receptor Antagonists mfano Cimetidine.

MATIBABU YA DAWA ZISIZO NA KEMIKALI (Food Suppliment)
⚡⚡Zipo dawa mbali mbali unazoweza tumia zikiwa kwenye mfumo wa unga au kimiminika ambazo hutibu vidonda vya tumbo vya aina yoyote ikiwemo sugu. Wasiliana nasi Eden Herbal & HealthCare kwa ushauri na tiba za maradhi mbali mbali

what'sApp /call/Text
+255 755 638 056
+255 784 467 374
Dr Peter - Mwanza

Comments

Popular posts from this blog

⚡FAIDA YA MBEGU ZA MABOGA⚡

🌳 JE, NINI HUMFANYA MTU KUWA NA HAMU YA KULA UDONGO? 🌳

ZIJUE FAIDA,MADHARA YA KITUNGUU SWAUMU KATIKA MWILI WA BINADAMU